Kuongeza Wingi na Ubora wa Mavuno yako
Maamuzi katika uchaguzi wa lishe ya mimea huchangia kwa kiasi kikubwa ustawi mzuri,wingi na ubora wa mavuno pia matokeo ya uzalishaji wa mazao kwenye mazingira.Tumia mbolea yenye kukusaidia kuyapa mazao yako lishe kamili na linganifu.
MiCROP Mbolea ya Kupandia
Mbolea bora kwa ajili ya kupandia mazao yote. (17N-29P-6K +7S+0.2Zn)%
- Inaepusha ukosefu wa virutubisho.
- Tumeboresha kanuni(fomula),ili kukidhi uhitaji wa virutubisho wa mazao yako,ikiwa imeboreshwa na YaraVita PROCOTE.
- Ina fosiforasi inayopatikana muda wote wa ukuaji wa zao.
MiCROP mbolea ya Kukuzia
Mbolea bora kukuzia mazao ya jamii ya nafaka kama vile mahindi,mpunga nk. na zao la miwa. (46N +0.2Zn)%
- Inahakikisha utoaji endelevu wa nitrojeni yenye uwezekano wa kutopotea haraka ardhini.
- Ikiwa imeboreshwa na YaraVita PROCOTE.
MiCROP MBOGAMBOGA
Ni mbolea ya mchanganyiko NPK iliyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ili kutoa lishe kamili na linganifu kwa ongezeko la wingi na bora wa viazi na mazao ya bustani(mbogamboga na matunda).
Virutubisho vilivyomo: 15%N:9%P2O5:20%K2O+8.5%S+0.01%B+0.06%Zn.
Faida za MiCROP MBOGAMBOGA
- MiCROP inatoa virutubisho 6 muhimu vyenye uwiano sahihi kwa mazao ya Mbogamboga na matunda.Inakupa thamani ya pesa yako.
- Tumeboresha kanuni(fomula),ili kukidhi uhitaji wa virutubisho wa mazao yako,ikiwa imeboreshwa na YaraVita PROCOTE.
- Kiwango kikubwa cha potasiamu wakati wa kukuzia muhimu kukidhi uhitaji wa mazao ya mbogamboga na matunda kwa mavuno mengi
- Huchochea utengenezwaji ngozi nyororo ya kupendeza na ubora wa ndani hasa kwa matunda na mazao jamii ya viazi.
- Inahakikisha utoaji endelevu wa nitrojeni yenye uwezekano wa kutopotea haraka ardhini.