Features
January 25, 2022

Yara: Kiongozi wa soko katika utoaji wa Programu za mbolea kwa wingi na ubora wa mazao.

Mbolea zetu ni zile zinazotoa lishe ya msingi inayohitajika zaidi ambayo ni; Nitrojen (N), Phosphorus (P) na Potassium (K), zinazochochea ukuaji na ubora wa virutubisho kama vile; Calcium (Ca) na Magnesium (Mg) na kutoa virutubisho vidogovidogo vinavyosaidia kuzuia au kutibu upungufu unaotokana na udongo au hali fulani ya mazao.


Yara: Kiongozi wa soko katika utoaji wa Programu za mbolea kwa wingi na ubora wa mazao.
Yara: Kiongozi wa soko katika utoaji wa Programu za mbolea kwa wingi na ubora wa mazao.

Wakati sehemu za kilimo zikiendelea kupungua kwa ukubwa kutokana na mgawanyo wa kimatumizi wa ardhi, kuna haja kubwa ya kuwa na ardhi inayotengwa kwa ajili ya kilimo cha mazao. Hii ni kwa sababu kuendelea kwa shughuli za kilimo katika ardhi hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi kunapunguza virutubisho muhimu vinavyohitajika kwa uzalishaji wa mazao.

Yara Tanzania ni kampuni tanzu ya Yara ASA ambayo imekuwepo na inafanya kazi kwa miaka zaidi ya 16 ikiingiza na kusambaza mbolea bora kwa kilimo.

Yara ni kiongozi mkuu wa soko Duniani yenye mbolea bora, maarifa na taaluma za kuongeza wingi na ubora wa mavuno na wakulima bora wananufaika kupitia kampuni hii huku wakipunguza athari za mazingira.

Imetengeneza mbolea maalumu ili kutoa lishe kamili na linganifu ya mazao mbalimbali. Yara pia inatoa programu za kuwajengea uwezo wakulima ikiwa na dhamira ya wazi ya kutoa huduma kwa wateja kwa ajili ya maendeleo ya kilimo kuanzia wakulima wadogo na wakubwa.

 

Mbinu tunayotumia

Kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, Yara imekusanya ujuzi usio na kifani katika lishe ya mazao. Vituo vyetu vimefanya maelfu ya majaribio na kukusanya aina zaidi ya milioni moja za udongo na uchanganuzi wa majani ya mimea ili kuongeza uelewa wetu katika kila aina ya mazingira ya kilimo, udongo na mazao. Sasa tuna masuluhisho yaliyothibitishwa ambayo yanatoa matokeo chanya kwa wakulima.

Upimaji wa udongo ni moja ya mambo muhimu tunayowahimiza wakulima kufanya mara kwa mara ili kuweka utaratibu mzuri wa mbolea kwa ajili ya mashamba yao. Tunafanya kazi na taasisi zinazotoa huduma za kupima udongo ili kutoa suluhisho bora la lishe ya mimea.

Mtandao wetu mpana wa wataalamu wa kilimo ulioenea kote nchini hutoa huduma za ugani kutoka kwenye matokeo ya uchambuzi wa udongo hadi uzalishaji wa mazao wakati wa msimu.

Afya bora ya udongo husaidia kuongeza wingi na ubora wa mavuno na uhifadhi wa muda mrefu wa mazao hivyo kuwezesha faida kubwa kwa wakulima.

 

Huduma tunayotoa

Yara tumetengeneza mbolea iliyochanganywa na yenye ubora wa hali ya juu unaolingana na mahitaji ya lishe ya mazao na kuhakikisha mpango wa lishe bora kwa mahitaji ya mimea.

Mbolea hizi huchaguliwa kwa uangalifu ili kuendana na hali ya mazingira ya nchi, mavuno na aina ya udongo na inapatikana kwa wakulima wadogo na wakubwa.

Mbolea zetu ni zile zinazotoa lishe ya msingi inayohitajika zaidi ambayo ni; Nitrojen (N), Phosphorus (P) na Potassium (K), zinazochochea ukuaji na ubora wa virutubisho kama vile; Calcium (Ca) na Magnesium (Mg) na kutoa virutubisho vidogovidogo vinavyosaidia kuzuia au kutibu upungufu unaotokana na udongo au hali fulani ya mazao.

Kwa hivyo, suluhu za kibunifu za mazao ambazo Yara Tanzania inatoa zina mchango mkubwa katika kufanikisha usalama wa chakula, kukuza uchumi na kuboresha maisha.