Features
January 25, 2022

Mbolea ya MiCROP Kuleta Mageuzi Katika Kilimo Cha Mahindi Na Mpunga

By: Jafari Juma, Mwananchi

Ujio wa mbolea ya MiCROP inayozalishwa na kuuzwa na kampuni ya Yara imekuja kuwa mkombozi kwa wakulima hawa kwani sasa wataondokana na kupata mavuno machache ya gunia saba kwa hekali na kuongezeka hadi kufikia gunia 30 shambani ama zaidi.


Mbolea ya MiCROP Kuleta Mageuzi Katika Kilimo Cha Mahindi Na Mpunga
Mbolea ya MiCROP Kuleta Mageuzi Katika Kilimo Cha Mahindi Na Mpunga

Sekta ya kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi.

Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara.  Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, mpunga nk.

Mazao hayo na mengine ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100.

Pamoja na kujitosheleza kwa chakula na kuchangia katika uchumi wa Taifa, takriban mazao yote hayo yamekuwa yakizalishwa kwa tija ndogo kwa maana ya kiasi cha mazao yanayozalishwa kwa eneo.

Aidha, uzalishaji umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mazao hayo kuzalishwa katika maeneo yaliyo nje ya ikolojia yake ya asili na ukosefu wa pembejeo bora ikiwemo mbolea.

Wakulima wengi kwenye kilimo cha mahindi na mpunga nchini wamekuwa wakikumbana na changamoto kwenye matumizi ya mbolea, ambapo wanatumia mbolea za mazoea mengine ambazo husababisha mavuno kuwa hafifu shambani.

Lakini ujio wa mbolea ya MiCROP inayozalishwa na kuuzwa na kampuni ya Yara imekuja kuwa mkombozi kwa wakulima hawa kwani sasa wataondokana na kupata mavuno machache ya gunia saba kwa hekali na kuongezeka hadi kufikia gunia 30 shambani ama zaidi.

Mbolea hiyo imekuja kuleta mageuzi makubwa kwa wakulima shambani kwani inawasaidia kuvuna mavuno zaidi pamoja na mazao kuwa na virutubisho aina tano tofauti ambavyo ni muhimu kwa ongezeko la tija kwenye kilimo cha mahindi.

Kampuni ya Yara Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa ya kuwajali wakulima nchini baada ya kuzindua ujio wa mbolea ya MiCROP na pia hutoa elimu ya shamba darasa kwa wakulima ili waweze kuongeza tija katika kilimo cha mkono.

Mbolea ya MiCROP imelenga kumnyanyua mkulima mdogo kuvuna mazao mengi shambani na wanawashauri wakulima ambao wanamitaji midogo kuanza kutumia mbolea hiyo.

Mkulima mwenye mtaji mdogo anashauriwa kuaanza na mbolea hii ya MiCROP na baadaye aende kwenye mbolea ya YaraMila OTESHA. Mbolea hii inachakatwa nchini na kiwanda kipo jijini Dar es Salaam hiyo yote ni kuwahudumia wakulima kwa karibu zaidi.

Mbolea ya MiCROP inavirutubisho vya Zinc na Sulphur Micronutrients ambazo zinahitajika kwenye mazao ili yaweze kuwa na viwango vyenye bora.

Kampuni ya Yara Tanzania, inayotengeneza na kusambaza mbolea ilizindua mbolea hii kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wa mahindi na mpunga kukuza mazao yao.

Mbolea hii mpya ilizinduliwa jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wasambazaji wa bidhaa za Yara nchini.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yara Tanzania, Winston Odhiambo alisema MiCROP ni mbolea yenye mchanganyiko wa virutubisho vya zinc na Sulphur vinavyohitajika na mmea katika mfumo huo na kutoa wito kwa wakulima wachangamkie mbolea hii kwa kilimo bora zaidi na kuongeza kuwa mbolea hiyo inasambazwa nchi nzima.

“Yara inazalisha mbolea zenye ubora zinazopatikana kila mahali na nyakati zote wakulima wa Afrika wanapozihitaji na inafanya kazi kwa ubia na taasisi za wakulima wenyeji,vikundi vya kijamii,na asasi zisizo za kiserikali kutoa elimu, majawabu ya lishe ya mimea na kuboresha maisha yao,” alisema Odhiambo.

Sifa za Mbolea ya MICROP

  • MiCROP ni mbolea bora ya kupandia na kukuzia mazoa hususani mahindi na mpunga.
  • Unaweza kutumia mfuko mmoja wa kilo 50 kwa ekari moja wakati wa kuotesha.
  • Unaweza kutumia mfuko mmoja wa kilo 50 kwa ekari moja wakati wa kukuzia.
  • Microp ni mbolea yenye virutubishi vingi kwa ajili ya kuoteshea/kupandia mazao yako
  • Ni mbolea yenye virutubisho vya aina tano (Nitrojeni, fosiforsi, potasiam, salfa na zinki), muhimu kwa ongezeko la tija kwenye kilimo cha mahindi.
  • Ni mbolea rafiki wa mazingira, inalinda ardhi kulingana na hali halisi ya udongo
  • Kwa wakulima wa mahindi wanashauriwa kutumia mfuko mmoja wa MiCROP mbolea ya kupandia, wakati wa kupanda. Mahindi yakifikisha majani 4-5- kuzia na MiCROP mbolea ya kukuzia
  • Microp ndiyo habari ya shambani kwa wakulima wadogo wa mahindi na mpunga.
  • Microp mbolea ya kukuzia inafanya vizuri hata kwenye uhaba wa mvua kuliko Urea.

Faida za kutumia MiCROP

  • Lishe linganifu; virutubisho vya aina tano (Nitrojeni, fosiforsi, potasiam, salfa na zinki). Muhimu kwa ongezeko la tija kwenye kilimo cha mahindi
  • Ukuaji wa mizizi; uwepo wa zinki unasaidia ukuaji haraka wa mzizi na kusimika zao/mmea vizuri na uchukuaji.

 

Asante!